Monday, 10 August 2015

TAZAMA BWANA TUNAKUJA KWAKO



TAZAMA BWANA TUNAKUJA KWAKO

Tazama, Bwana tunakuja kwako (leo)
Twaleta sadaka yetu mbele yako
Tunakuomba Mungu Baba pokea *2

·  Kwa nguvu zako tuliweza kustawisha
Mazao bora, na sasa twakutolea
Mashamba uliyarutubisha kwa
mvua nzuri mazao mengi yakasitawi
·  Bahari mito na maziwa Bwana ukajaza
Samaki wengi wa kupendeza
Angani ndege wengi wanarukaruka
kushangilia neema yako ee Bwana
·  Wanyama maporini wanarukaruka
Kushangilia neema yako ee Bwana
Wadudu nao wakachezacheza kuonyesha
Furaha kubwa waliyo nayo

No comments:

Post a Comment