NAKUJA NA ZAWADI
Naondoka
mimi naenda kwa Baba,Nipeleke hiki nilichokipata,
Japo kidogo, sitaona haya,
Nimeamua, sitarudi nyuma
Nakuja polepole Baba,
Nakuja na zawadi yangu
Naleta mbele zako
Ili nitoe shukurani *2
Nakuja na zawadi yangu
Naleta mbele zako
Ili nitoe shukurani *2
- Natembea mimi mwendo wa madaha,
Nakanyaga chini kwa maringo tele,
Naelekea altare ya Bwana,
Nimkabidhi nilichojaliwa. - Nimechangamka ninashangilia,
Napiga kelele, kelele za shangwe
Nachezacheza, najongea kwako,
Ee Mungu Baba Nipokee mimi. - Nafsi yangu mimi naileta kwako,
Mkate divai, pia ninaleta
Uigeuze mwili na damuyo,
Chakula chetu, tunaosafiri - Mavuno shambani mimi nimevuna,
Mifukoni fedha nimekabidhiwa,
Mimi ni nani, nisikushukuru,
Baba nasema asante kwa yote.
No comments:
Post a Comment