NIKUPE
NINI EE MUNGU
- Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza
Uwezo wangu mdogo Bwana waujua
Pamoja na dhiki inayonisonga
Pokea zawadi yangu hii duni - Nikitazama wenzangu wanakutolea
Zawadi nyingi na nzuri za kukupendeza
Kasoro mimi tu natoa kidogo
Wakati mwingine sitoi kabisa - Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua
Unyonge na udhaifu wangu waujua
Sina kitu mimi cha kukutolea
Lakini pokea nafsi yangu Bwana - Nayakabidhi maisha yangu kwako Bwana
Uniongoze katika njia za uzima
Unisaidie wakati wa shida
Kwani ni wewe tu tumaini langu - Kutoa ndugu ni moyo sio utajiri
Ukimtolea Mungu atakuongeza
Uwasaidie watu maskini
Wasiojiweza utabarikiwa - Ninawasihi wenzangu mliojaliwa
Maisha bora mazuri na ya kuridhisha
Msimsahau Bwana Mungu wenu
Toeni kwa wingi mtabarikiwa.
No comments:
Post a Comment