Monday, 10 August 2015

MISA AMECEA- UTUKUFU



MISA AMECEA - UTUKUFU
  Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani kote duniani
(Kwa watu) wenye mapenzi mema

|s/a| Tunakusifu Baba, tunakuheshimu,
Twakuabudu sisi tunakutukuza
|t/b| Kusifu tunakusifu, heshimu,
Twakuabudu abudu tunakutukuza

  Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu
Wako mkuu ewe Mungu mfalme
(Ee Baba) wa Mbingu Baba yetu

  Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu
Mwana wa pekee wake Mungu
(Uliye) Mwanakondoo wa Mungu

  Unayeziondoa dhambi zote
Za dunia utuhurumie
(Pokea) pokea ombi letu
  Wewe unayeketi kuume
Kwake Baba utuhurumie
(Sikia) sikia ombi letu

  Kwani pekee yako ndiwe Bwana
Pekee yako mkuu na mkombozi
(Pekee) pekee Yesu Kristu

  Kwa umoja wa Roho mtakatifu
Ndani yake Baba watukuzwa
(Ee Yesu) milele na milele

No comments:

Post a Comment